Spurs kupiga panga wachezaji 11
TIMU ya Tottenham Hotspur inapanga kupitisha panga la nguvu, hatua itashuhudia 11 wa kikosi cha kwanza wakiondoka.
Kocha wa Spurs Ange Postecoglou anataka kujenga timu hiyo iliyoshika nafasi ya 5 Ligi Kuu England(EPL) msimu uliopita, ambayo imepata nafasi kucheza Ligi ya Europa na sasa anapanga mabadiliko katika klabu hiyo.
Ripoti ya tovuti ya The Standard ya England imewataja miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuuzwa dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi ujao kuwa ni pamoja a Emerson Royal, Bryan Gil, Pierre-Emile Hojbjerg, Giovani Lo Celso, Joe Rodon, Djed Spence, Sergio Reguilon, Tanguy Ndombele na Japhet Tanganga.
Postecoglou amesema mabadiliko lazima yafanyike iwapo klabu hiyo ya London Kaskazini inataka kushidana katika mashindano mbalimbali msimu ujao ikiwemo kushika nafasi 4 za juu EPL na kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya.