Simba Queens wakabidhiwa chao mapema
DAR ES SALAAM; MABINGWA Wapya wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, Simba wamekabidhiwa kombe la Ubingwa baada ya mchezo wao dhidi ya Geita Queens.
Simba Queens ameibuka na ushindi wa mabao 3-0 mchezo uliopigwa uwana wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam.
Mshambuliaji Aisha Mnuka alianza kuifungia Simba Queens dakika 3 baada ya pasi tamu ya Ritticia Nabbosa na bao la pili limefungwa na Elizabeth Wambui dakika ya 34 na Asha Rashid ameifungia bao la tatu dakika 79,
Simba Queens wanafikisha mechi 18 bila kupoteza na kutoa sare mchezo mmoja na Bunda Queens, wakiwa tayari mabingwa kwa pointi 52 kwa misimu minne.
Wekundu hao wa Msimbazi wametwaa ubingwa huo kwa kuwapoka JKT Queens wameshindwa kutetea taji hilo kwa kumaliza msimu wakiwa na pointi 43.
Mbali na ubingwa huo, mshambuliaji Aisha Mnuka amefanikiwa kufikia kutwaa tuzo ya ufungaji bora amemaliza ligi akifunga mabao 20 akimpiku Stumai Abdallah amemaliza na mabao 18.
Kikosi cha Simba, Carolina Rufa, Fatima Suleiman, Diana Mnaly, Daniella Ngoyi, Violeth Nicholaus, Vivian Corazane, Ritticia Nabbosa, Aisha Juma, Jentrix Shikangwa, Asha Djafar na Elizabeth Wambui.
Geita Queens: Florida Osundwa, Mariam Salum, Lucia Patrick, Husna Badru, Tabea Aidano, Onesta Kindawi, Restuta Innocent, Teddy Safari, Alice Sébastien, Sabina Alex na Patricia Salum .
Michezo mingine iliyocheza leo kwenye viwanja mbalimbali hapa nchini, Yanga dhidi ya Alliance Girls 1-0, Amani Queens ameshunda mabao 5-0 dhidi ya Baobab Queens, JKT Queens ameshinda 2-0 dhidi ya Ceasiaa Queens na Fountain Gate Princess 1-0 Bunda Queens