Ligi Kuu

Yanga kuwakosa Bacca, Depu dhidi ya TRA

ARUSHA: Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Concalves amesema mapokezi makubwa waliyoyapata kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo walipowasili jijini Arusha yamewapa nguvu na motisha zaidi ya kuendelea kupambana katika michezo ijayo.

Kupitia ujumbe wake, kocha huyo amesema sapoti na upendo mkubwa waliouonesha mashabiki umeongeza morali kwa wachezaji na benchi la ufundi, huku akisisitiza kuwa kikosi hicho kitaendelea kuwa imara na kupambana kwa ajili ya wale wanaokiunga mkono.

“Mapokezi mazuri kutoka kwa Wananchi baada ya kuwasili Arusha yametupa nguvu kubwa. Kuhisi upendo na sapoti hii kunatupa motisha zaidi. Tutaendelea kuwa imara, wamoja na kupigana kwa ajili ya wale wanaotuunga mkono,” amesema Conclaves.

Ameongeza kuwa kikosi hicho kitaendelea kukabiliana na changamoto zote kinazokutana nazo huku kikizidi kuwa imara kadri msimu unavyoendelea.

Conclaves amesisitiza kuwa umoja ndani ya timu pamoja na sapoti ya mashabiki ndiyo nguzo muhimu itakayoiwezesha Yanga kufanya vizuri katika michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga ipo Arusha kwa ajili ya maandalizi ya mchezo ujao wa ligi dhidi ya TRA utakaochezwa kesho huku ikitangaza kuwakosa wachezaji wake tegemeo kama Ibrahim Bacca aliyepata jeraha la nyonga, Laurindo Aurelio ‘Depu’ jeraha la nyama za paja, Chadrack Boka jeraha la enka mguu wa kushoto na Edmund John aliumia bega.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button