Ligi Kuu

Gamondi awakingia kifua wachezaji

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema ugumu wa ratiba ni sababu ya baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kushindwa kuwa kwenye daraja lililozooleka.

Akijibu swali la waandishi wa habari kuhusu kushuka kiwango kwa nyota Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho kocha huyo amesema hawawezi kuwa katika ubora kwa wakati wote.

Amesema anaridhishwa na kiwango cha wachezaji wake inawezekana kuna nyakati mambo hajaendi sawa lakini haangalii mchezaji mmoja mmoja huwa anaangalia zaidi matokeo ya timu.

“Mchezaji kuwa na siku mbaya kazini ni kawaida duniani kote hata wachezaji wa Ulaya mfano Kylian Mbape, hata hivyo naridhika na mwenendo wa wachezaji wangu wote.

Sina wasiwasi kabisa na timu yangu, sijui hayo yanatoka wapi kama unajua mpira huwezi kuwa na mashaka na Yanga nafikiri wale  wanajiuluza uliza maswali watapata majibu, muda utaongea,” amesema Gamondi.

Kuhusu mchezo wa kesho dhidi ya Pamban Jiji, amesema ratiba sio rafiki sana ya wachezaji kujiandaa na kuwa na utimamu wa kimwili, wapo tayari kwa mchezo huo. Anajua wanakutana na mchezo mgumu .

Ameeleza kimsingi hawapati shida sana kwa kuwa wamejipanga kiakili na kimwili wapo imara .

Related Articles

Back to top button