Africa
Yanga kama mlivyosikia

DAR ES SALAAM: KLABU ya Yanga imeondoshwa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya MC Alger katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini.
Kwa matokeo hayo MC Alger imefuzu hatua ya robo fainali akiwa na alama tisa, Yanga akivuna pointi nane na Al Hilal anaongoza kundi hili akiwa na pointi 10.
Dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza kimetamatika Yanga 0-0 MC Alger katika mchezo, Wananchi wamefika langoni kwa wapinzani mara kwa mara na kutengeneza nafasi moja iliyolenga lango na nne hazikulenga.
Sasa Mabingwa hao wa soka nchini wanarejea kuendelea na michuano ya ndani.