AfricaKusini Mwa Afrika

Twiga Stars mwendo mdundo COSAFA

Kikosi cha Twiga Stars kilichoanza katika mchezo dhidi ya Comoros leo.

MABINGWA watetezi wa taji la Ubingwa wa Vyama vya soka Kusini mwa Afrika(COSAFA) Timu ya taifa ya soka ya wanawake(Twiga Stars)leo baada ya kuichapa Comoros mabao 3-0.

Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Madibaz uliopo jiji la Port Elizabeth, Afrika Kusini.

Nyota wa Twiga Stars Enekia Lunyamila alikuwa mwiba kwa Comoros akifunga mabao mawili katika dakika za 41 na 51.

Twiga ilianza kufungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Donisia Minja katika dakika ya 13 ya mchezo.

Wawakikishi hao wa Tanzania COSAFA watashuka tena dimbani kwa ajili ya mechi yake ya pili Septemba 5.

Twiga Stars ipo kundi C la michuano hiyo pamoja na Botswana, Malawi na Comoros.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button