Yanga majaribuni shirikisho leo


KLABU ya Yanga leo inashuka dimbani kuikabili Club Africain ya Tunisia katika mchezo wa kwanza kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
Mchezo huo utafanyika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Yanga iliangukia hatua hiyo baada ya kutolewa na Al Hilal ya Sudan hatua ya awali kufuzu makundi Ligi ya mabingwa Afrika.
Mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu wa 2021/2022 wanahitaji kucheza karata yao vizuri kwa ushindi mnono utakaowaweka katika nafasi nzuri katika mchezo wa marudiano.
Mchezo wa marudiano utafanyika Tunisia Novemba 9, 2022.
Mechi nyingine za michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika leo ni kama ifuatavyo:
Flambeau du Centre vs Motema Pembe
Rivers United vs Al-Nasr
Royal Leopards vs AS Real Bamako
TP Mazembe vs Royal AM
Rail Club de Kadiogo vs Saint-Eloi Lupopo
ASKO vs CS Sfaxien
Djoliba AC vs FAR Rabat
Plateau United vs Al Akhdar
Primeiro de Agosto vs Future
ASN Nigelec vs Pyramids
ASEC Mimosas vs Sporting Gagnoa
Cape Town City vs USM Alger
Al Ahli Tripoli vs Marumo Gallants
US Monastir vs RSB Berkane