Africa

Yanga inapiga palepale

DAR ES SALAAM: TIMU ya Yanga ya Tanzania imeanza vizuri michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji wao Vital ‘O ya Burundi.

Mchezo huo ni wa mkondo wa kwanza wa Ligi hiyo uliochezwa uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam, ambapo Vital’ O wakitumia kama dimba la nyumbani kutokana na kwao kutokuwa na kiwanja chenye hadhi ya kimataifa.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo yamefungwa na Stephane Aziz Ki dakika ya 90 kwa penati, bao la tatu limefungwa na Clement Mzize, Prince Dube na Clatous Chama.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button