Wema: Sijawahi kumsaliti mpenzi wangu

DAR ES SALAAM: MSANII wa filamu nchini, Wema Sepetu, amesema hajawahi kuchepuka wala kumsaliti mpenzi wake, akisisitiza umuhimu wa kuwa mwaminifu katika mahusiano.
Wema ametoa kauli hiyo kupitia mitandao ya kijamii alipokuwa akijibu ujumbe wa mmoja wa wafuasi wake kuhusu suala la kuchepuka katika mahusiano.
Katika majibu yake, Wema ameweka wazi msimamo wake akieleza kuwa hajawahi kufanya usaliti kwa mwenza wake, huku akisisitiza kuwa kwake uaminifu ni jambo muhimu katika mahusiano.
Kauli hiyo imekuja baada ya mmoja wa wafuasi wake kueleza kuwa kwake kitendo cha kucheating ni jambo linalohitaji juhudi, jambo lililomfanya Wema kueleza mtazamo wake kuhusu uaminifu.
Wema amekuwa akishirikisha mara kwa mara mambo mbalimbali kuhusu maisha yake kupitia mitandao ya kijamii, huku kauli zake zikivuta hisia na maoni kutoka kwa mashabiki na wafuasi wake.
Katika ujumbe huo, msanii huyo hakueleza zaidi kuhusu mahusiano yake ya sasa, bali alisisitiza msimamo wake kuhusu suala la uaminifu kwa mwenza.
Kauli hiyo imeibua mneno miongoni mwa wafuasi wake kuhusu umuhimu wa uaminifu na mawasiliano katika kujenga mahusiano.




