Ligi Daraja La Kwanza

Walter Harson: Utendaji bora ulinileta Yanga

MENEJA wa Yanga, Walter Harson amesema utendaji wake bora kwenye tasnia ya habari ni sababu ya Rais wa Yanga, Hersi Said kumpa ulaji klabuni hapo.

Julai 31, 2022 Yanga ilitangaza kumuajiri Walter Harson kuwa meneja wa klabu hiyo.

Akizungumza na mtandao huu, Walter Harson amesema utendaji wake ulianza kuonekana akiwa Azam TV ambako alikuwa mchambuzi wa michezo na baadaye klabu ya KMC kama Mkurugenzi Mtendaji kisha kuajiriwa Yanga.

“Hakuna njia rahisi yoyote iliyokuweka kwa mimi kuweza kufika hapa, lakini ni juhudi ambazo nimeweza kuzifanya za utendaji,” amesema Walter.

Pia meneja huyo amesifu idara zingine ndani ya klabu hiyo kwa namna zinavyoendelea kupiga hatua nzuri kila kukicha, ikiwemo idara ya fedha, habari, sheria na zingine.

Related Articles

Back to top button