Ligi Daraja La Kwanza

Gamondi-Uwiano wa timu ni wachezaji kutegemeana

KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema matokeo chanya ya sasa ya klabu hiyo yanatokana na jitihada za wachezaji na benchi la ufundi.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandhishi wa habari leo Dar es Salaam kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara Septemba 20, Gamondi amesema amejenga mazingira ya kuwa na timu yenye uwiano mzuri kwa kila idara ndio maana Yanga imefunga magoli mengi lakini imeruhusu goli moja tu katika michezo saba tena bao la penati ambalo ilikuwa kosa la timu yake.

Kocha huyo raia wa Argentina amesema jambo alilozingatia kwanza ni wachezaji kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe, wachezaji kuheshimu falsafa zake na kwamba kocha hawezi kuwa mzuri kama wachezaji hawamheshimu.

“Sasa ili uwe na uwiano na namna hiyo lazima ujenge timu inayotegemeana na sio timu inayomtegemea mtu fulani kwenye idara fulani,” amesema Gamondi.

Amesema dira yake sio sio mchezaji mmoja mmoja bali timu nzima na ndio maana timu yake inacheza mchezo mzuri, na mchezaji yoyote anaweza kufunga.

Gamondi amesema baadhi ya wachezaji wana uchovu na wengine wana majeraha lakini ana imani na waliopo benchi kwa sababu anajua wanaweza kuleta matokeo chanya.

Related Articles

Back to top button