Tetesi
Wapeni Rashford mpewe Osimhen

Manchester United wana mpango wa kubadilishana mchezaji wao Marcus Rashford na mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen. Rashford, ambaye ni zao la akademia ya Manchester United, anaweza kuwa sehemu ya dili la kubadilishana wachezaji huku United wakimlenga Osimhen kama mbadala wake.
Kwa mujibu wa taarifa za The Sun, United wako tayari kutoa kiasi kikubwa cha fedha kumnunua Osimhen, lakini wanatumaini kupunguza gharama hiyo kwa kumjumuisha Rashford kwenye mazungumzo.
Ikiwa mpango huo utafanikiwa, Rashford ataelekea kucheza chini ya kocha Antonio Conte huko Napoli, ambako atakutana na mshambuliaji wa zamani wa United, Romelu Lukaku, pamoja na mchezaji mwenzake wa zamani, Scott McTominay.