Tetesi

Haaland katika rada za Barcelona

TETESI za usajili zinasema mshambuliaji wa Manchester City raia wa Norway, Erling Haaland ni mlengwa wa uhamisho wa Barcelona katika majira ya kiangazi 2025.

Wakala wa Haaland, 23, Rafaela Pimenta, amekutana na mkurugenzi wa michezo wa Barcelona, Deco mwezi uliopita. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Jose Mourinho amesema yupo tayari kurejea kwenye ukocha majira yajayo ya kiangazi baada ya kuondoka Roma.(Fabrizio Romano)

Liverpool na Bayern Munich zimeonesha nia kumteua kocha wa Brighton Roberto de Zerbi awe mbadala wa kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso. (Bild – in German)

Wolves inaongoza mbio kumsajili mshambuliaji wa Southampton na Scotland Che Adams, 27, atakapokuwa huru majira yajayo ya kiangazi. (Telegraph – subscription)

Ajax inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo mwingereza wa Aston Villa,Tim Iroegbunam, 20. (Football Insider)

Brighton inamfuatilia winga wa Nigeria Philip Otele, 24, anayekipiga katika klabu ya Cluj ya Romania.(Evening Standard)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button