Tetesi za usajili

KIUNGO mshambuliaji Bernardo Silva amefanikiwa kujadiliana kuhusu kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 50 sawa na shilingi bilioni katika mkataba wake mpya Manchester City na anafikiria kuhamia Barcelona mwaka 2024.(Mundo Deportivo)
Manchester United imepewa ofa ya kumsajili winga aliye huru Anwar El Ghazi lakini haina nia ya dili hilo. Huku Antony and Jadon Sancho kwa sasa hawako kwenye kikosi cha kwanza, kocha Erik ten Hag anatarajiwa kuwategemea Facundo Pellistri, Alejandro Garnacho, Bruno Fernandes na Mason Mount kucheza wingi ya kulia.(The Athletic)
Mshambuliaji ajaye wa Real Madrid Endrick Felipe Moreira de Sousa, maarufu Endrick wa Palmeiras ya Brazil amekiri kuwa atamkaribisha Kylian Mbappe katika klabu hiyo ya Hispania, ambaye anatarajiwa kuondoka Paris Saint-Germain kwa uhamisho huru msimu ujao.(TNT Sports)
Nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard amekataa kutoa taarifa mpya kuhusu mazungumzo ya mkataba lakini amesisitiza ana furaha sana katika klabu hiyo. (Nettavisen)
Liverpool wako katika harakati kuhusu uwezekano wa kumsajili winga wa PSV Eindhoven Johan Bakayoko, Januari 2024. Mbelgiji huyo alikataa ofa kujiunga na Brentford majira ya kiangazi.(Football Insider)
Barcelona na Real Madrid zitagombea saini ya nyota wa Argentina, Federico Redondo ambaye ni mtoto wa kiungo wa zamani, Fernando. (Fichajes)