Nyumbani

Vyama 61 vya michezo kufutwa Iringa

IRINGA: VYAMA vya Michezo 61 mkoani Iringa vipo hatiani kufutiwa usajili kwa kutofuata matakwa ya uendeshaji michezo nchini.

Kwa mujibu wa kaimu msajili wa vyama vya michezo nchini ( BMT ), Evordy Kyando katika mkutano na wadau wa michezo mkoani hapo, amevitaka vyama  kujinasua katika sakata la kufungiwa.

Ametaja sababu kuu zinazosababisha chama kukosa haki ya kuendelea kuwepo ni pamoja na kutolipa ada kwa mujibu wa miongozo iliyowekwa, kutofanya mashindano mbalimbali, kutofanya mikutano kwa mujibu wa katiba ya chama na kutowasilisha hesabu za mapato na matumizi.

“Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na idadi ya vyama visivyokuwa hai, bora kuvifuta na kusajili vipya ambayo vitaweza kufuata matakwa. Nia ni njema ya kuendeleza michezo nchini” amesema.

Kyado amesema wadau wenye nia ya kuvinusuru vyama vyao waje kwenye Baraza kwani wapo tayari muda wote kwa ajili ya kuwasaidia na kuvifanya vyama hivyo kuwa hai na kuendelea na shughuli za kuendeleza michezo nchini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button