Kocha wa Kiduku akoshwa na wacheza soka

MOROGORO: KOCHA wa bondia Twaha Kiduku, Chanzi Mbwana ‘Power Iranda’ amesema jambo linalofanywa na wachezaji wa soka nchini kucheza mechi za hisani ni jambo linalopaswa kuigwa na wachezaji wa michezo mingine
Aliyasema hayo siku ya jumamosi mkoani Morogoro kwenye mchezo wa hisani kati ya Timu Kibwana na Timu Job,
Kocha Mbwana alisema kitendo cha kusaidia jamii ni sehemu ya kuwaweka karibu mashabiki, hivyo amewataka wadau wa sekta ya mchezo wa ngumi, mapromota na mabondia kufanya jambo kama hilo kwa jamii kama wanavyofanya wachezaji wa mpira wa miguu Tanzania.
Kauli hiyo ameitoa siku ya jumamosi baada ya kushuhudia tamasha la Wape tabasamu lililoandaliwa na nyota wawili wa Yanga, Shomari Kibwana na Dickson Job kwa kushirikisha wachezaji wenzao na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi.
Akizungumza na Spotile, kocha alisema kwa macho ya kawaida unaona kitendo kinachofanywa na wachezaji hao ni dogo lakini kubwa sana na kujiweka karibu na jamii ambayo wapo nyuma yao.
Alisema jambo hilo limezoeleka kufanywa na wachezaji wa mpira wa miguu kwa kuwepo kwa tamasha kubwa, wamefanya kitu kikubwa na kinatakiwa kuigwa kwa tasnia ya michezo mingine.
“Kuiga sio dhambi hasa kitendo cha kujiweka karibu na jamii ambayo inakupa sapoti katika kazi zako, huyo shabiki anatumia nguvu na kipato chake kwa ajili yetu lakini tutambue kuwa jamii hiyo ina matatizo mengi.”
Vilevile alisema jamii Zina matatizo mengi ambayo yanapaswa kutafutiwa ufumbuzi.
“Kuna matatizo kama kuchangia mahitaji muhimu katika Hospitali kama ilivyo kwa wachezaji hao wa mpira miguu, sasa kazi iliyopo mapromota na mabondia kuangalia jambo la kuweza kurejesha kwa jamii” alisema kocha Mbwana