MICHEZO mitano ya raundi ya 3 Kombe la Shirikisho la Azam(ASFC) inafanyika leo kwenye viwanja tofauti.
Mkoani Mwanza, Ihefu ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Mbuni ya Arusha kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
Azam na Green Warriors zote za Dar es Salaam zitaonesha kazi kwenye uwanja wa Azam Complex wakati Geita Gold itaikaribisha Mbeya City kwenye uwanja wa Nyankumbu, Geita.
Nyamongo kutoka mkoa wa Mara itakuwa mgeni wa Tabora United kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
JKT Tanzania itakuwa uwanja wa nyumbani wa Mej Jen Isamuhyo kuikaribisha TMA Stars ya Arusha.
Katika michezo miwili ya kombe hilo iliyofanyika Februari 21 Mtibwa Sugar imeichapa Stand United mabao 3-2 wakati Namungo imeibamiza Transit Camp mabao 3-1.