Kwingineko
USELESS FACT : WOTE WAMEJERUHIWA SIKIO

MAREKANI: Kushoto ni Bingwa wa zamani wa uzito wa juu wa masumbwi (WBA) Evander Holyfield akiwa na Mshauri wa Fedha wa zamani wa Mike Tyson na Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump.
Kwa nyakati tofauti za maisha yao, wote wamepata jeraha la sikio.
Katika pambano la marudiano mnamo Juni 28, 1997 Mike Tyson alimuuma sikio Evander raundi ya tatu ya pambano na kutoka na kung’oa sehemu ya sikio baada ya Mike kukubali kichapo kikali cha mbwa mwizi.
Upande wa mpeperusha bendera ya Republican katika kinyang’anyiro cha Urais wa Marekani mwaka huu, Trump yeye tukio lake bado bichi kabisa kwani habari kubwa ulimwenguni leo ni kumhusu yeye kujeruhiwa kwa risasi sikioni akiwa katika kampeni katika Jimbo la Pennsylvania.