Unai aapa kuirejesha Aston Villa Champions League

BIRMINGHAM:KOCHA wa Aston Villa Unai Emery amesema kikosi chake kitarejea tena kwenye Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu ujao baada ya kuondoshwa kwenye hatua ya robo fainali katika michuano hiyo usiku wa kuamkia leo.
Aston Villa wanashikilia nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England wakiwa na pointi 54 point moja nyuma ya Manchester City wanaoshika nafasi ya 5 ambayo msimu ujao itakuwa na nafasi ya kufuzu moja kwa moja kwenye michuano hiyo yenye msisimko wa aina yake duniani.
“Ninajivunia sana tulichofanya msimu huu kwenye Champions League, sasa ni muhimu turejee tena msimu ujao. Michuano muhimu zaidi kwetu kwa sasa ni Champions League tuna kazi ya kufanya kwenye ligi ili turejee huku, tuna kila sababu na nia ya kufanya hivyo kwenye mechi 6 zilizosalia” amesema Unai
Aston Villa sasa wanatafuta nafasi ya kuwa wenyeji wa michuano hiyo baada ya kukosekana kwenye michuano hiyo kwa karibu miaka 40. Na hawakurejea kinyonge baada ya kuwa ‘Surprise package’ msimu huu ikiduwaza vigogo kadhaa wa soka la Ulaya.