Kwingineko

UCL, UEL kazi tena leo

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya(UCL) na Ligi ya Europa(UEL) hatua ya 16 bora inaendelea leo kwa michezo mitatu.

Bingwa mtetezi wa UCL, Manchester City itaikaribisha FC Copenhagen kwenye uwanja wa Etihad, City ikiwa imeshinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-1.

RB Leipzig itakuwa mgeni wa Real Madrid kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, Real ikiwa imeshinda mchezo wa kwanza kwa bao 1-0.

Tayari Paris Saint-Germain na Bayern Munich zimefuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuzitoa Real Sociedad na Lazio.

Katika Ligi ya Europa Sporting CP itakuwa mwenyeji wa Atalanta kwenye uwanja wa Jose Alvalade uliopo mji mkuu wa Ureno, Lisbon.

Related Articles

Back to top button