Nyumbani

Mkutano Mkuu Simba Jan 21

Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu ya Simba utafanyika Dar es Salaam Januari 21, 2024.

Taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imesema ajenda za mkutano huo ni kama zilivyoainishwa katika ibara ya 22 ya Katiba ya Simba ya mwaka 2018.

“Aidha kufuatia maelekezo ya Baraza la Michezo la Taifa(BMT), moja ya ajenda itakayojadiliwa na mkutano mkuu ni mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya Simba Sports Club,” imesema Taarifa hiyo.

Simba imesema bodi imeunda kamati maalum ya wajumbe saba kuratibu mchakato wa marekbisho ya katibu kwa mujibu wa mapendekezo ya BMT na maoni ya wananchama.

Related Articles

Back to top button