Wachezaji Ujerumani kujichanga nauli za mashabiki wao

MAREKANI:WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Ujerumai watatoa sehemu ya posho zao kulipia gharama za usafiri kwa mashabiki 600 watakaosafiri kwa basi mpaka uwanja MetLife katika mji wa New Jersey ambako timu hiyo itacheza mechi yake ya mwisho ya Kundi E dhidi ya Ecuador Juni 25, mwaka huu .
Ujerumani wanafanya hivyo kuwapunguzia mzigo mashabiki wao kutokana na gharama kubwa za usafiri wa umma nchini Marekani wakati huu wa Kombe la Dunia ambapo nauli katika treini na basi zimepanda kwa zaidi ya mara nne kutokana ugeni mkubwa wa mashabiki wa kandanda kutoka sehemu tofauti za dunia wanaomiminika nchini humo kwa ajili ya michuano hiyo.
Usafiri wa basi ambao awali ulikuwa unagharimu dola 12.9 sawa na sh. 33,798 za Tanzania,sasa unagharimu hadi dola 98 za kimarekani sawa na sh. 256,760. ikiwaa ni punguzo kutoka dola 150 ambazo zilikuwa zimepangwa na serikali ya marekani kwa ajili ya kombe la dunia,sawa na sh.393,000.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Ujerumani,nahodha wa timu hiyo ya taifa,Joshua Kimmich na wachezaji wote watachangia gharama hizo.




