LIGI Kuu Tanzania Bara inaendeleo leo kwa mchezo mmoja kufanyika jijini Tanga.
Wenyeji Coastal Union itaikaribisha Geita Gold kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Coastal inacheza uwanja wa nyumbani ikitoka kupoteza mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate kwa mabao 2-1 wakati Geita ina kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata dhidi ya Namungo katika mchezo ulopita.
Geita Gold ipo nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 13 baada ya michezo 11 wakati Coastal inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 10.