Ligi Kuu

Singida: Ubora wetu unatupa imani dhidi ya JKT

DAR ES SALAAM:OFISA Habari na Mawasiliano wa Singida Black Stars, Hussein Massanza, amesema maandalizi ya timu hiyo kuelekea mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania yanaendelea vizuri huku kikosi kikiwa na morali ya juu ya kupata matokeo chanya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Massanza amesema wanaifahamu na kuiheshimu JKT Tanzania, lakini wanaamini ubora wa kikosi chao unawapa sababu ya kuingia uwanjani wakiwa wanajiamini.

“Maandalizi yanaendelea vizuri. Hakuna ugumu wowote wa kukutana na JKT Tanzania. Tunawaheshimu, lakini ubora wetu unatufanya tujiamini na tunaamini tuna ubora kuliko wao,” amesema Massanza.

Alibainisha kuwa timu hiyo imebakiwa na michezo mitano muhimu katika mbio za kumaliza msimu, huku kila mchezo ukiwa na uzito mkubwa katika kufikia malengo waliyojiwekea.

Massanza amesema lengo kuu la Singida Black Stars ni kuhakikisha inapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao, jambo linalowalazimu kupambana kwa nguvu zote katika michezo iliyosalia.

Kauli hiyo inaonyesha namna Singida Black Stars ilivyojipanga kuhakikisha inamaliza msimu kwa nguvu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutimiza ndoto ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button