
KLABU ya Mashujaa ya Kigoma imemtangaza na kumtambulisha Abdallah Mohamedi Barres kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo.
Barres alikuwa akiifundisha Tanzania Prisons hadi mwisho wa msimu uliopita wa 2022/2023.
“RASMI ABDALLAH BARRES NI SHUJAA. Kocha Abdallah Mohamedi Barres ndio atakuwa anaingoza timu yetu kama Kocha Mkuu kwa kandarasi ya mwaka mmoja,”imesema taarifa ya Mashujaa.
Mashujaa imepanda daraja kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/2024 ikiitoa Mbeya City katika michezo miwili mtoano kwa jumla ya magoli 4-1.