Kwingineko

TIKA yakabidhi uwanja shule ya msingi Mseto

DAR ES SALAAM: Katika kukuza vipaji vya michezo, Shirika la Maendeleo la Uturuki (TIKA) lililopo nchini limekabidhi uwanja wa michezo kwa Shule ya Msingi Mseto iliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam, ili kukuza soko la michezo, ambalo kwa sasa lina manufaa na kupendwa na wengi.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, wakati wa makabidhiano hayo na kusema kuwa uwanja huo utunzwe ili uweze kuwa na manufaa kwa vijana.

Mwinjuma amesema yote hayo yametokana na mahusiano mazuri na ushirikiano baina ya Tanzania na Uturuki, hivyo vitaibua vipaji kwani michezo ni sehemu muhimu kwa taifa letu.

“Miongoni mwa maeneo tunayofanya vizuri sana ni michezo, hivyo tunatambua na tunaendeleza vipaji kwa kadri vinavyopatikana ili wawe wachezaji wakubwa, wajiajiri wao wenyewe kupitia michezo na waweze kuliwakilisha taifa letu siku za usoni,” amesema Mwinjuma.

“Ndiyo maana ninaposema suala la Mbwana Samatta, na Samatta wengine, mimi roho yangu inaridhika sana kwa sababu hicho ndicho tunachojaribu kulifanya kwa sasa,” ameongeza Mwinjuma.

Kwa upande wake, Rais wa Shirika la TIKA, Bekir Gezer, amesema uwanja huo umetengenezwa katika kuadhimisha miaka 100 ya nchi yao na ni sehemu ya kumbukumbu hiyo, pia kudumisha mashirikiano baina ya nchi zote mbili.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button