Tetesi

Man United yawinda saini ya Timo Werner

TETESI za usajili zinaeleza kuwa klabu ya Manchester United imemchunguza mshambuliaji wa kijerumani wa RB Leipzig, Timo Werner mwenye umri wa miaka 27 na Januari 2024 inaweza kutuma ombi la kumsajili.(Sky Sports Germany)

Arsenal inafanya mpango wa kumsajili kiungo Mbrazil, Douglas Luiz, anayekipiga Aston Villa mwenye umri miaka 25.(ESPN). Manchester City na Liverpool pia zina nia kumsajili Luiz.(90 Min)

Hata hivyo, Kocha wa Aston Villa, Unai Emery amesema klabu hiyo haikusidii kumuuza Luiz.(Standard)

Manchester City na Arsenal zinavutiwa na fowadi wa kitaliano, Francesco Camarda wa klabu ya AC Milan mwenye umri wa miaka 15.(Tuttosport – subscription, in Italian)

Newcastle United inaweza kumsajili kwa mkopo Januari 21, 2024 mshambuliaji wa kifaransa anayecheza Paris Saint-Germain, Hugo Ekitike.(Caught Offside)

Related Articles

Back to top button