Tetesi

Liverpool haijakata tamaa kwa Mbappé

TETESI za usajili zinaonesha Liverpool haijakata tamaa ya kumsajili fowadi Kylian Mbappé kwa uhamisho huru kutoka Paris Saint-Germain mwisho wa msimu huu lakini inatambua ushindani wa Real Madrid ambayo pia inamwania mchezaji huyo.(L’Equipe)

Manchester United inaweza kutuma ombi kumsajili golikipa wa Porto, Diogo Costa kufuatia wasiwasi wa kumpoteza André Onana kwenda katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Januari 2024.(Todo Fichajes)

Barcelona bado inawania saini ya kiungo wa Ujerumani, Joshua Kimmich, ambaye huenda asisaini mkataba mpya Bayern Munich.(Fichajes)

Kocha Jurgen Klopp anataka Liverpool kumsajili fowadi wa Borussia Dortmund, Donyell Malen, awe mbadala wa Mohamed Salah, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi akifikiriwa kugharimu pauni milioni 50.(Todo Fichajes)

Arsenal inafikiria uhamisho wa kiungo wa Royal Antwerp, Arthur Vermeeren kwa ada ya pauni milioni 13 Januari 2024 lakini inakabiliwa na upinzani kutoka Barcelona.(SPORT)

Related Articles

Back to top button