
TETESI za usajili zinasema Juventus inaongoza mbio kumsajili fowadi wa Manchester United na England, Mason Greenwood, 22, ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Getafe ya Hispania. (i Sport)
Kocha wa Barcelona, Xavier Hernández Creus ‘Xavi’ ameiambia klabu hiyo kwamba anamhitaji kiungo wa Manchester City na Ureno, Bernardo Silva, 29, lakini pia Bayern Munich ina nia kumsajili. (Sport – in Spanish)
Manchester United ipo mbele katika mbio za kumsajili kiungo wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 21, Michael Olise, 22. (ESPN)
Chelsea inafikiria kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Poland na golikipa wa zamani wa Arsenal, Wojciech Szczesny, 34, ambaye sasa anakipiga Juventus. (Tutto Juve – in Italian)
Manchester City ni miongoni mwa timu zilizomfuatilia beki wa kati wa kidachi anayekiwasha Chelsea Mei Mosi, Ian Maatsen, 22, ambaye yupo kwa mkopo Borussia Dortmund. (TBR Football)