Filamu

Tamasha la MAMI Mumbai latangaza filamu zitakazoshindanishwa 2024

MUMBAI: TAMASHA la MAMI Mumbai limetangaza kufanyika kuanzia Oktoba 19 hadi 24 huku likiweka wazi filamu na vipengele vitakavyoshindanishwa katika tamasha hilo.

Tamasha hilo maarufu zaidi barani Asia, litakalofanyika kwa siku sita likijikita kwenye filamu za kimataifa, ubunifu na utamaduni mbalimbali linatarajiwa kuonyesha zaidi ya filamu 110 kutoka nchi zaidi ya 45 zikijumuisha lugha zaidi ya 50.

Shindano la mwaka huu linajumuisha vipengele 11 vyenye uwakilishi mzuri wa filamu saba za Asia Kusini na diaspora, pamoja na vipengele vinne vya Kihindi. Safu hii ina mchanganyiko wa hadithi za kubuni, matukio halisi na uhuishaji pamoja na filamu zilizotayarishwa pamoja kimataifa na utayarishaji binafsi.

Waongozaji watano kati ya wanaoshindana ni wanawake na filamu nyingi ni Maonyesho ya Kwanza ya Asia ya Kusini na safu inayojumuisha duniani kote, Asia na India.

Filamu zinazowakilisha lugha zaidi ya 10 na kutoka nchi 12, shindano hili linakuza vipaji vipya huku ikitetea ubunifu na mabadiliko ya sinema.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button