Tajiri katajwa tena huko
DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Rais wa heshima wa klabu ya Simba Sports club ya jijini Dar es Salaam, Mohammed Dewji (Mo) ametajwa na jarida la Face2Face Africa lenye makao makuu yake jijini New York nchini Marekani kuwa mmoja kati ya mabilionea wawili ambao wamesaidia kukuza biashara ya mpira wa miguu barani Afrika.
Taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa rasmi za klabu hiyo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam imesema Kutajwa kwa Mo Dewji kumetokana uwekezaji na mafanikio ambayo Simba imeyapata tangu alipoanza kufanya uwekezaji katika klabu hii kubwa zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Tangu mwekezaji huyo aanze kuwekeza katika klabu hiyo Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mara nne mfululizo na kucheza mara tano hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF
Simba pia imefanikiwa kushika nafasi ya saba kwa ubora wa vilabu barani Afrika.