Ligi KuuNyumbani

Wageni wanavyozidi kuipaisha Ligi Kuu Bara

WACHEZAJI wa kigeni wamekuwa wakiipa thamani kubwa Ligi Kuu Tanzania Bara, kutokana na uwezo, kiwango na hata vituko vyao wakati mwingine.

Mfano msimu uliopita kipa wa Yanga, Djigui Diarra aliibuka kipa bora kwa msimu wa pili mfululizo na aliingia pia kwenye kinyanganyiro cha mchezaji bora wa ligi kabla ya tuzo hiyo
kuchukulia na Fiston Mayele, ambaye naye ni wa nje.

Kwa misimu uliyopita nyuma haikuwa kitu rahisi kwa mchezaji wa nafasi ya kipa tena raia wa kigeni kupendekezwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa msimu lakini ilitokea kwa Diarra kutokana na uwezo wake aliouonesha akiwa na jezi ya Yanga.

Mbali na Diarra lakini tunaona katika upande wa ufungaji bora ni Saido Ntibazonkiza na Mayele wote wakiwa raia wa kigeni ndio walioibuka washindi wa tuzo hiyo kila mmoja
akifunga mabao 17.

Ukitafuta mchezaji mzawa aliyefunga angalau nusu ya mabao hayo kwa timu zote 16, itakuwa ngumu kumpata hiyo inadhihirisha wazi kuwa wachezaji wa kigeni wanamchango mkubwa katika ligi yetu.

Ukiachana na hayo hata mchezaji aliyeongoza kwa kutoa pasi za mwisho za mabao msimu uliopita ni kiungo wa Simba, Clatous Chama raia wa Zambia ndiye aliyetoa pasi nyingi za
mwisho.

Kwa faida yako hata misimu miwili nyuma mchezaji bora wa Ligi Kuu alikuwa ni Yannick Bangala raia wa DRC Congo hivyo ni wazi uwepo wa wachezaji wakigeni kwenye ligi yetu
unaonekana kwa tija kubwa zaidi.

Katika kipindi cha misimu minne iliyopita Simba ya Tanzania imekuwa kinara kwa kushiriki mara kwa mara na kuishia hatua ya robo fainali huku ikizifunga timu vigogo Afrika, hapa
nazungumzia Al Ahly, Kaizer Chiefs, Orolando Pirates, Wydad Casablanca na nyinginezo na imekuwa ikipata matokeo.

Nguvu hizo ni kutokana na mchango mkubwa wa wachezaji wakigeni mfano bao alilolifunga Chama kwenye mchezo dhidi ya Nkana FC ya Zambia vile vile huwezi kulisahau bao la Chama huyo huyo dhidi ya AS Vita pale Benjamin Mkapa.

Mchango na wingi wa wachezaji wakigeni leo hii ndio umechangia Simba kuwepo kwenye timu nane zitakazo shiriki michuano maalumu ya Super League ambayo inashirikisha timu bora zilizokuwa na mwendelezo mzuri kwenye michuano ya kimataifa.

Achana hilo la Simba msimu uliopita Yanga ilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika katika safari hiyo kipa Diarra raia wa Mali aliibuka mchezaji bora wa mechi na anatajwa kuwa ndio kipa bora wa mashindano.

Lakini mshambuliaji Mayele ndio kinara wa mabao kwenye michuano hiyo akifunga mabao saba katika mechi 12 alizoichezea Yanga, kuanzia hatua ya makundi, hii inaonesha namna gani wachezaji wa kigeni wingi na uwepo wao umekuwa na faida kubwa kwa soka la Tanzania.

Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania (TFF), nalo linahusika katika hilo kwa kuzirihusu klabu kusajili wachezaji 12 wakigeni lengo likiwa kuziongezea ubora na ushindani.

Wazo hilo limeonekana kulipa kwa kiasi kikubwa ndio maana leo Ligi Kuu ya Tanzania Bara, inatajwa kuwa ligi inayoshika namba tano Afrika kwa ubora na hiyo imefanya kuwavutia
wachezaji wengi wakigeni pamoja na makocha kuja kucheza soka sababu wanaamini watapata ushindani mzuri na malipo mazuri.

Mchezaji kama Skudu Makudubela, kutoka Afrika Kusini, Stephene Aziz Ki, Willy Essomba Onana na Jose Luis Miquissone walikubali kuha nchini kutokana na ubora wa ligi ulivyo na
hakuna kingine.

Tuje kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2023/24, ambao tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo timu zilizokuwa na uwezo wa kusajili wachezaji wakigeni ni Simba, Yanga na Azam msimu ujao imekuwa tofauti.

Klabu nyingi ikiwemo Singida Fountain Gate, Tabora United, Mashujaa, Ihefu, Namungo, KMC, Coastal Unioni na hata Tanzania Prisons zimesajili wachezaji wakigeni na wengi wao wanauwezo mkubwa na wametoka timu kubwa Afrika hiyo inaonesha kwamba ujio wao utaongeza ushindani kwenye ligi yetu.

Na kama itakuwa hivyo basi ushiriki wa timu za Tanzania kwenye michuano ya kimataifa utakuwa wa ushindani na haitokuwa ajabu kuanzia msimu ujao kuona timu moja kutoka Tanzania ikibeba taji la Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho.

Sababu klabu zimefanya usajili wa wachezaji wakubwa timu kama Singida Fountain Gate imemsajili kiungo tegemezi wa Rivers United Morris Chuwkhu lakini Tabora United imemsajili aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Enyimba ya Nigeria John Noble.

Hii inathibitisha kwamba Ligi ya Tanzania inakwenda kuongezeka ushindani kutokana na ujio wa wachezaji hao wakigeni lakini wingi wa wachezaji hao wa kigeni utakwenda kusaidia kuwabusti wazawa kuongeza juhudi ili kugombania nafasi za kucheza kikosi cha kwanza kwenye timu zao.

TFF chini ya Rais Wallace Karia imekuwa na maono ya mbali kuruhusu klabu kusajili
wachezaji 12 wa kigeni hiyo imesaidia sana kuona ligi ya Tanzania kufatiliwa na watu wengi Afrika na hata Ulaya.

Related Articles

Back to top button