Africa

Simba yaenda Luanda na ‘Mpunga’

DAR ES SALAAM: Kikosi cha Simba kimeondoka leo kuelekea Angola katika mchezo wa ugenini dhidi ya Bravos do Maquis utakaochezwa Jumapili, Januari 12,  uwanja wa 11 de Novembro, Luanda nchini humo huku uongozi wa klabu hiyo ukitoa ahadi nzito.

Kaimu Mkurugenzi Mtandaji Mkuu wa Simba, Zubeda Hassan amesema amefanya mazungumzo na benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids na wachezaji,  maandalizi yanaenda vizuri na wameenda kusaka ushindi dhidi ya Bravos do Maquis.

“Tumeandaa mazingira mazuri kwa ajili ya wachezaji wanaenda kupambana katika mchezo huo kutafuta alama muhimu kama ilivyokuwa kwa Tunisia na CS Sfaxien.

“Nimewaahidi wachezaji wetu safari hii ya Luanda haitakuwa ya maneno matupu, tumeandaa mazingira mazuri ya uwezeshi kwa ajili ya kuwapa hamasa wachezaji wetu kusaka alama ushindi ugenini,” amesema.

Simba ipo nafasi ya pili na alama 9 sawa na CS Constantine wanaongoza kundi A, Bravos do Maquis nafasi ya tatu na alama sita na Cs Sfaxien wanashika mkia hawana alama.

Related Articles

Back to top button