Ateba, Mukwala kuja kivingine
DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amewataka washambuliaji wake Leonel Ateba na Steven Mukwala kuwa makatili zaidi mbele ya lango la wapinzani.
Kauli hiyo ya Fadlu ni kufuatia ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya FC Bravos katika mchezo Kundi A, Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Jumanne, Novemba 27 jijini Dar es Salaam.
Fadlu amesema washambuliaji wanatakuwa kuwa na uchu na kutumia vizuri nafasi wanazopata kutafuta ushindi mnono katika michezo iliyopo mbele yao.
“Mechi iliyopita tulitengeneza nafasi nyingi, washambuliaji wangekuwa makatili kwenye eneo la ulinzi tungeshinda mabao mengi.
Tunahitaji kuimarika licha ya kupata matokeo ya alama tatu, tunahitaji kufanya mabadiliko kwa washambuliaji kwani mashindano yatakuwa magumu zaidi,” amesema.
Fadlu amesema wanaendelea na mazoezi kujiandaa na maandalizi ya mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho ugenini dhidi ya CS Constantine kwa ajili ya kutafuta matokeo chanya.
Simba inatarajia kucheza mchezo huo Desemba 8, nchini Algeria.