Africa
Yanga kutinga makundi CAFCL?
KLABU ya Yanga leo inashuka dimbani katika mchezo wa marudiano kuwania kufuzu makundi Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan.
Mchezo huo utafanyika uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Kigali Pele, Rwanda Septemba 16, Yanga ilishinda kwa mabao 2-0.
Matokeo ya suluhu, sare ya mabao ya idadi yoyote au kufungwa bao lisizozidi moja katika mchezo wa leo yataipeleka moja kwa moja Yanga makundi ya michuano hiyo.