Ligi Kuu

Simba kukipiga Uwanja wa Uhuru Ligi ya Mabingwa

DAR ES SALAAM: Timu ya Simba imethibitisha kuwa itautumia Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) hatua ya makundi.

Hiyo, ni baada ya kukubali masharti na vigezo vilivyowekwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Meneje wa Habari wa Simba, Ahmed Ally, ameeleza kuwa CAF imetoa idhini hiyo ya wao kuendelea na matumizi ya uwanja huo baada ya kufanya ukaguzi uwanjani hapo na kujiridhisha.

Awali kulikuwa na sitofahamu ya uwanja gani Wekundu hao watautumia kuelekea michuano hiyo lakini sasa uwanja huo umekidhi baadhi ya vigezo vinavyotakiwa kwenye viwanja vinavyotumika kwa ajili ya mechi za hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Hivi karibuni, pia ziliibuka taarifa za pengine Simba ingeelekea Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa ajili ya mechi hizo lakini sasa imedhihirika kuwa hilo halipo tena.

Hata hivyo, Ahmed Ally amesema Simba imekubaliana na masharti na vigezo hivyo vya CAF, akisisitiza kwamba timu yao itautumia uwanja huo kwa ajili ya michezo yote ya Kundi C lenye timu nyingine za Orlando Pirates, RS Berkane na Colombe Sportive.

Related Articles

Back to top button