Ligi Kuu

Pacome: Safari ya kupona inaendelea 

DAR ES SALAAM: KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua, ameelekea nchini Ufaransa kukamilisha awamu ya mwisho ya matibabu na urejeshaji wa utimamu wa mwili baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na jeraha kubwa la mguu.

Pacome amethibitisha hatua hiyo kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, akieleza kuwa safari yake ya kupona inaendelea na sasa anaanza hatua ya mwisho ya matibabu yake nchini humo.

“Baada ya kipindi kigumu kilichotawaliwa na jeraha, safari ya kupona inaendelea. Leo ninaelekea Ufaransa kuanza hatua ya mwisho ya matibabu yangu,” amesema Pacome.

Ameeleza kuwa mchakato huo haukuwa rahisi, lakini umemfundisha kuwa mvumilivu, mwenye ustahimilivu na kutokukata tamaa katika kukabiliana na changamoto.

“Haikuwa safari rahisi, lakini kila hatua imenifundisha uvumilivu, ustahimilivu na nguvu ya kutokukata tamaa. Ninaendelea kuwa makini, mwenye dhamira na mwenye shukrani kwa wote ambao wamekuwa nami na kuniunga mkono katika kipindi hiki kigumu,” amesema.

Pacome alipata jeraha hilo Juni 29, 2026, katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu msimu wa 2025/26 dhidi ya JKT Tanzania, uliochezwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo. Yanga ilishinda 3-0 na kutwaa ubingwa wa tano mfululizo, lakini ushindi huo uliambatana na huzuni baada ya kiungo huyo kuumia mguu na kuondolewa uwanjani kwa msaada wa gari la wagonjwa.

Related Articles

Back to top button