Kwingineko

Blueface akana kumwibia bondia Broner

CALIFORNIA: RAPA Blueface amekanusha uvumi kuwa kundi lake lilimwibia Adrien Broner, baada ya bondia huyo kuonekana kupoteza fahamu au kutojitambua katika tamasha moja jijini Los Angeles ambapo Blueface alitumbuiza mwishoni mwa wiki.

Imeelezwa kuwa begi Broner linadaiwa lilikuwa na kiasi cha kati ya Dola 50,000 na 100,000, na liliibwa wakati akiwa katika hali hiyo ya kupoteza fahamu.

Blueface ambaye pia ni bondia, anasema madai hayo hayana ukweli wowote, akisisitiza kuwa hajui chochote kuhusu kilichompata Broner au kilichotokea kwa begi lake.

Alisema hajawahi kumuona Broner katika hali kama hiyo hapo awali, jambo lililomtisha kidogo.

Aliongeza kuwa Broner hakuweza hata kupanda jukwaani pamoja naye kwa sababu alionekana katika hali ya ‘kuchanganyikiwa sana.’

Wakati wa tukio, Blueface alikuwa akifanya matangazo ya moja kwa moja mtandaoni na kumuonesha Broner akiwa amedondoka kwenye kochi, akiwa amepoteza fahamu kabisa.

Marafiki wa Broner walimsaidia kumshusha katika ngazi na kumweka kwenye kiti cha magurudumu. Baadaye, wahudumu wa afya walimsukuma Broner hadi kwenye gari na kumuingiza ndani.

Related Articles

Back to top button