AFCON

Taifa Stars yatua Nigeria, kazi kuanza

LAGOS: TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imewasili nchini Nigeria tayari kwa mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya wenyeji wao.

Kuwasili kwa kikosi hicho kunaashiria hatua nyingine ya maandalizi kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, huku benchi la ufundi likiwa na jukumu la kuhakikisha wachezaji wanakuwa tayari kukabiliana na changamoto ya kucheza ugenini.

Taifa Stars itashuka dimbani Novemba 13 mwaka huu kuvaana na Nigeria katika Uwanja wa Godswill Akpabio, uliopo Uyo, kabla ya timu hizo kukutana tena Novemba 17 katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.

Baada ya mchezo wa kwanza, Stars itarejea nyumbani kwa ajili ya marudiano, ambako itahitaji kutumia vizuri faida ya kucheza mbele ya mashabiki wake ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupata matokeo inayoyahitaji.

Licha ya tayari kufuzu, matokeo hayo yana umuhimu katika viwango vya kimataifa lakini pia, kwa wachezaji kuonesha ubora wao na mchango wao kuelekea fainali za Afrika mwakani nchini Tanzania, Kenya na Uganda.

 

Related Articles

Back to top button