LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kufanyika Singida na Lindi.
Ihefu inayoshika nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 20 baada ya michezo 18 itakuwa mwenyeji wa KMC iliyopo nafasi ya 5 ikiwa na pointi 25 baada ya michezo 19.
Kwenye uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi, Kagera Sugar iliyopo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 23 baada ya michezo 19 itakuwa mgeni wa Namungo inayoshika nafasi 10 ikiwa na pointi 20 baada ya michezo 18.