Sheffield yakubali bil 57/- kumsajili Archer

SHEFFIELD United ‘The Blades’ iliyapanda Ligi Kuu England(EPL) imekubali dili kumsajili fowadi wa Aston Villa, Cameron Archer kwa ada ya pauni milioni 18.5 sawa na shilingi bilioni 57.3, ripoti zimesema.
The Blades inahitaji kuboresha safu ya ushambuliaji huku kocha Paul Heckingbottom akiwategemea zaidi Benie Traore na Will Osula katika mechi mbili za mwanzo EPL.
Kwa sasa mafowadi wakongwe Oli McBurnie na Rhian Brewster ni majeruhi wakati klabu hiyo ya Yorkshire imemuuza Iliman Ndiaye katika klabu ya Marseille mapema majira haya ya kiangazi na habari kuhusu Archer zitaleta faraja kwa mashabiki wa Sheffield.
Sheffield United itaikaribisha Manchester City Agosti 27 huku The Blades ikitumaini kukamilisha dili hilo kwa wakati ili acheze dhidi ya mabingwa wa EPL.