Tetesi

Man United yafikiria kumsajili Olise

TETESI za usajili zinasema Manchester United inafikiria kumsajili winga wa Kifaransa anayecheza Crystal Palace, Michael Olise, 22. (90min)

Manchester United pia inataka kumsajili beki wa Brazil, Gleison Bremer, 26, kutoka Juventus majira yajayo ya kiangazi. (Calciomercato – in Italian)

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona,Deco ameripotiwa kuandaa orodha ya wachezaji 5 inaotaka kuwasajili kuelekea dirisha la uhamisho majira ya kiangazi.(dailymail)

Wachezaji hao ni Gabriel Martinelli, Amadou Onana, Kaoru Mitoma, Khvicha Kvaratskhelia na Aleix Garcia.(dailymail)

Manchester City inamfuatilia kiungo wa West Ham na Brazil Lucas Paqueta, 26. (Football Insider)

Related Articles

Back to top button