Tetesi

Joao Felix akaribia Barca kwa mkopo

KLABU ya Atletico Madrid imemruhusu fowadi Joao Felix kuhamia Barcelona kwa mkopo kukiwa na kipengele cha chaguo la kumnunua.

Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya soka, 90min, Barcelona inaona dili ‘haliwezekani’ kwa wakati huu na itajaribu kumsajili Felix kwa ‘masharti yenye punguzo’.

Mapema wiki hii Felix amekiri kwamba ingekuwa ndoto yake kucheza Barcelona.

“Ningependa kucheza Barca. Siku zote Barcelona imekuwa chaguo langu la kwanza na ningependa kujiunga na Barca. Siku zote imekuwa ndoto yangu tangu nikiwa mtoto, iwapo itafanyika, ndoto yangu itakuwa imetimia,” amesema Felix.

Ili nafasi ya kumsajili Feliz iwepo, Barcelona inaweza kuwapeleka katika timu ya Atletico Madrid, Franck Kessie na Ferran Torres kama sehemu ya dili. Kwa sasa Kessie anahitajika Juventus.

Related Articles

Back to top button