Nyumbani

Seleman Mwalimu ajivunia kuweka historia baada ya kuifunga Yanga

ZANZIBAR: KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Seleman Mwalimu, amesema anajivunia mafanikio aliyoyapata baada ya kufunga bao muhimu katika mchezo wa dabi, akisisitiza kuwa ameandika historia ambayo haitasahaulika kirahisi.

Mwalimu alitoa kauli hiyo mara baada ya mchezo huo mgumu uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0 na Simba kuchukua ubingwa wa Muungano.

Amesema kuwa licha ya furaha aliyonayo, anatambua uzito wa mafanikio hayo katika maisha yake ya soka.

“Nina furaha lakini naamini katika maisha yangu nimeweka historia, na historia isiyofutika. Kufunga katika dabi sio rahisi,” amesema Mwalimu.

Ameongeza kuwa ushindi huo umechangiwa kwa kiasi kikubwa na sapoti ya mashabiki wa Simba waliojitokeza kwa wingi uwanjani kuipa nguvu timu yao.

“Kikubwa namshukuru Mungu, na naamini wanasimba wamefurahi, wamefika kwa wingi kuisapoti timu yao,” ameongeza.

Mwalimu aliibuka pia mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga mabao matatu.

Related Articles

Back to top button