Ligi Ya WanawakeNyumbani
Simba vs Yanga: Dabi ya kisasi Ligi Kuu wanawake
LEO ni leo katika dabi ya Kariakoo Ligi Kuu ya wanawake Tanzania Bara kati ya Simba Queens na Yanga Princess.
Mchezo huo pekee wa ligi hiyo leo utafanyika uwanja wa Azam Complex,uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa mara mwisho timu hizo zilikutana nusu fainali ya Ngao ya Jamii wanawake Desemba 9, 2023 Simba Queens ikiitoa Yanga Princess kwa mikwaju ya penalti.
Matokeo ya michezo mingine ya Ligi Kuu wanawake iliyopigwa Januari 2 ni kama ifuatavyo:
Amani Queens 0 – 10 JKT Queens
Alliance Girls 0 – 1 Fountain Gate Princess
Baobab Queens 1 – 1 Bunda Queens
Ceasiaa Queens 2 – 1 Geita Gold Queens