Kwingineko

Samatta gari limewaka Ligue 1

PARIS, Ufaransa: MSHAMBULIAJI wa Tanzania, Mbwana Samatta amefunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) akiwa na timu yake ya Le Havre.

Mchezaji huyo wa zamani wa Genk ya Ubelgiji ameandika historia nyingine ya kuwa Mtanzania wa kwanza ambaye amefanikiwa kufunga goli katika ligi kuu kubwa mbili barani Ulaya ambapo alifunga goli kwenye Ligi Kuu England (EPL) akiwa na Aston Villa na amefunga goli Ligue 1 nchini Ufaransa akiwa na timu ya Le Havre.

Katika mchezo wa jana Samatta alifunga bao la kwanza akiwa na jezi ya Le Havre katika mchezo dhidi ya Nice uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Tangu Samatta alipojiunga na Le Havre katika dirisha kubwa la usajili la majira ya kiangazi alikuwa hajaifungia timu hiyo hadi alipofanya hivyo jana.

Katika mechi hiyo, Samatta alifanyiwa mabadiliko katika dakika ya 87 akimpisha Stephan Zagadou.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button