EPL

“Salah ni mbinafsi” Gallagher

LONDON: Mchezaji wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya England Jamie Gallagher ameonesha kusikitishwa na kauli ya winga wa klabu  ya Liverpol, Mohammed Salah ambaye alisema Liverpool hawajayapa uzito mazungumzo ya kuongeza mkataba wake unaomalizika mwishoni mwa msimu huu.

Salah aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Southampton kuwa Liverpool hawajaonesha nia ya mazungumzo yeyote ya kumuongeza mkataba.

Kauli hiyo imemuibua Gallagher ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa kituo cha televisheni cha Sky Sports cha nchini England aliyesema kuwa maoni ya mchezaji huyo ni ya ‘ubinafsi’

“Liverpool wana michezo migumu wiki hii, wana mchezo dhidi ya Real Madrid katikati ya wiki na Manchester City wikiendi hiyo ndio story kwa Liverpool hivi sasa”

“Kitu muhimu zaidi kwa Liverpool hivi sasa sio mustakabali wa Mo Salah, sio wa Virgil Van Dijk sio mustakabali wa Trent. Kitu cha muhimu zaidi ni Liverpool kushinda Premier League hiyo ndio muhimu kuliko mchezaji yeyote”

“Akiendelea kujizungumzia kipindi kama hiki au meneja wake kuendelea ‘kutweet’ kuzungumzia hilo suala huo ni ubinafsi, ni kujifikiria wao wenyewe na si klabu” amesema Gallagher

Mo Salah mwenye miaka 32 amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu zaidi kwenye kikosi cha majogoo wa Liverpool ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu huu

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button