Rudeboy, Ifeoma wanatarajia mtoto

ABUJA, Nigeria: MWANAMUZIKI Paul Okoye, anayejulikana pia kwa jina la Rudeboy, anatarajia kupata mtoto wa kwanza na mke wake mpya, Ivy Ifeoma.
Rudeboy mwenye miaka 42 na mkewe huyo mwenye miaka 24 wanatarajia mtoto wa kwanza baada ya mapema mwaka huu kufunga ndoa ya kitamaduni.
Ifeoma ndiye wa kwanza kuweka picha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha kuwa mjamzito na kuandika neno “Mungu.”
Rudeboy, alioa tena miaka mitatu baada ya kutengana na aliyekuwa mke wake Anita Okoye. Wanandoa hao wa zamani wana watoto watatu.
Kabla ya ndoa na matarajio hayo ya kupata mtoto wa kwanza kwao, Ifeoma alionyesha kuumia kwake baada ya kuhisiwa kwamba alikuwa na uhusiano na Rudeboy wakati alipokuwa na Anita ingawa Rudeboy alikanusha tuhuma hizo huku akidai baada ya kutoa talaka hakuwa katika mahusiano na yeyote kwa takribani miaka minne.
“Unanifahamu, huwa naweka mambo yangu kimya. Sikusema kwa muda mrefu, nimekuwa ‘single’ ndipo nikampata Ifeoma ambaye sasa ndiye mke wangu sikuwahi kumuona kabla ya muda huo,” alieleza Rudeboy.