Kwingineko

River Plate yamlilia Mastantuono

WASHINGTON, Kocha wa River Plate Marcelo Gallardo amesema uhamisho wa mchezaji wake Franco Mastantuono kwenda Real Madrid umekuja mapema sana, hususan wakati huu kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 bado alikuwa akiimarika na ni muhimu kwa ustawi wa klabu yake.

Gallardo amekiri kuondoka kwa Mastantuono kutaacha pengo kubwa katika kikosi chake baada ya wababe wa Spain Real Madrid kukamilisha dili la takriban dola milioni 45 na River kwa ajili ya kinda huyo mapema mwezi huu.

Kocha huyo raia wa Argentina, ameiambia ESPN kuwa kiungo huyo bado alihitaji muda zaidi kukua ndani ya klabu hiyo lakini alikubali kuwa uhamisho huo wa mapema ni sehemu inayoeleweka ya soka la kisasa.

“Ni kawaida, tunawafunza wachezaji kwa ajili ya ulimwengu. Kila kitu kinatokea mapema, wachezaji wachanga wanaondoka haraka, na ninaelewa kuwa hizo ndizo sheria za mchezo,”

“‘Project’ yetu ya michezo kwa mwaka huu alikuwa yumo. Inabidi turekebishe, kwa sababu kuna wachezaji ambao kwa asili yao ni vigumu kuziba pengo lao, wachezaji kama Mastantuono. Gallardo aliiambia ESPN

Kocha huyo pia amesema anaendelea kumsihi Mastantuono aweke akili yake kwenye mechi za michuano ya Kombe la Dunia la Klabu na azipuuze kelele zinazoendelea nje juu ya uhamisho wake ambao mashabiki wengi hawajapenda.

Related Articles

Back to top button