Angus MacInnes afariki dunia

NEW YORK: MUIGIZAJI maarufu, Angus MacInnes aliyetamba katika filamu ya Star Wars: A New Hope aliyoshiriki kwa jina Jon ‘Dutch’ Vander, amefariki dunia akiwa na miaka 77.
Familia yake imetangaza kifo chake katika ukurasa rasmi wa Facebook wa mwigizaji huyo jana.
Familia hiyo ilieleza kwamba MacInnes aliaga dunia Desemba 23, 2024, lakini hawakuweka wazi sababu ya kifo chake.
MacInnes alizaliwa Oktoba 27, 1947, huko Ontario, Canada. MacInnes alifurahia kazi yake ya uigizaji ambapo ameonekana katika filamu mbalimbali mashuhuri duniani ikiwemo ‘Witness’, ‘Judge Dredd’, ‘Hellboy’ na ‘Captain Phillips’ Pamoja na kuwa kiongozi wa waasi wa kikosi cha Y-wing katika ‘Star Wars: A New Hope’.
“Angus alikuwa zaidi ya mwigizaji, alikuwa mtu mkarimu, mwenye mawazo na mkarimu ambaye alileta uchangamfu na ucheshi katika maisha ya kila mtu aliyemfahamu,” familia iliandika. “Kazi yake iligusa maisha mengi na ataendelea kujivuni kuwa sehemu ya hadithi zinazoendelea kusimuliwa kwa mema na watazamaji wake ulimwenguni pote,
“MacInnes alikuwa na uhusiano maalum na jamii ya Star Wars, mashabiki wa Star Wars walikuwa na nafasi maalum moyoni mwake kwa maana alikuwa mnyenyekevu, mtu wa kufurahisha, kuheshimisha na alivutiwa na mashabiki zake,” ilieleza taarifa hiyo.
Kufuatia tangazo hilo, mashabiki walimiminika kwenye mitandao ya kijamii na kumuenzi muigizaji huyo wakimsifu kwa uigizaji wake wa kukumbukwa. Wengi walisherehekea mchango wake katika sakata ya Star Wars na furaha aliyoleta kwa mashabiki ulimwenguni kote.